Miaka mitano baada ya kupita kimya box office, Those Who Wish Me Dead ya Jon Bernthal na Taylor Sheridan sasa ni hit kubwa Netflix, ikithibitisha kuwa adult thrillers bado zina nguvu.
Kuna aina ya movie ambazo Hollywood ilizoea ku-deliver bila shida — star mkubwa, premise ya hatari, villains wachache wa kutisha, na dakika 100 za action bila kuchezeana. Those Who Wish Me Dead (2021) ni movie ya aina hiyo, na ingawa ilipita kimya box office ikiwa na collection ya karibu dola milioni 23 tu duniani kote, sasa miaka mitano baadaye imegeuka kuwa moja ya movies zinazoongoza kutazamwa Netflix Marekani.
Hii ni neo-Western thriller ya Taylor Sheridan (yule yule wa Yellowstone na Wind River), ikiwa na cast kali: Angelina Jolie kama Hannah Faber, smoke jumper anayemkuta Connor (Finn Little), mtoto wa miaka 12 anayewindwa na wauaji wawili professional baada ya baba yake kuuawa. Jon Bernthal anacheza Ethan Sawyer, sheriff wa eneo hilo na mjomba wa Connor, ambaye anajikuta ndani ya mchezo hatari huu wa maisha na kifo. Nicholas Hoult na Aidan Gillen nao wapo kwenye cast, wakileta uzito wa villains.
Setting yenyewe ndiyo inayofanya kila kitu kuwa intense — Montana Wilderness, ambapo msitu mkubwa unatoa nafasi ya kujificha lakini pia unawapa wawindaji nafasi ya kufuatilia. Kisha moto wa msituni unaanza kuenea, na ghafla tatizo halibaki tu ni wauaji, bali ni survival dhidi ya wildfire inayokula kila kitu njiani. Ndio maana Sheridan anaonyesha ustadi wake wa neo-Western — badala ya farasi na miji ya frontier, anatumia helicopters, smoke jumpers na moto wa mwitu kuunda hatari ile ile ya zamani ya lawman anayelinda mtu dhaifu dhidi ya maadui wanaomkaribia.
Kwa nini movie kama hii zilipotea Hollywood? Mabadiliko ya TV ndiyo chanzo kikubwa — networks kama HBO, FX na AMC zilianza kuchukua nafasi ya thriller stories kupitia prestige TV series, hivyo studios zikaanza kuwekeza zaidi kwenye IP zenye franchise tayari-established badala ya original stories zenye stars tu. Movie kama hii, isiyo na superhero wala sequel number, ikawa gamble kubwa kwa studio yoyote.
Lakini Netflix imeondoa vizuizi vyote hivyo — hakuna tiketi ya kununua, hakuna kusita kuhusu kwenda sinema kutazama title usiyoifahamu. Ipo tu kwenye orodha, ikishindana na mamia ya titles nyingine, na jina la Jolie, Bernthal na Sheridan pamoja na thriller ya dakika 100 yenye survival na moto — inatosha kufanya iwe easy choice kwa watazamaji leo.
Chanzo: ScreenRant