Ariana Grande na Cynthia Erivo wanaungana tena kwenye 'For Good' — track ya kufunga safari ya 'Wicked' kwa emotion ya hali ya juu.
Kama ulikuwa unasubiri closure ya musical journey ya Wicked, Wicked: For Good — The Soundtrack imeshafika, na track kuu "For Good" iliyoimbwa na Cynthia Erivo na Ariana Grande ndiyo centerpiece.
Soundtrack hii ina-feature songs zote maarufu za Act 2 ya stage show ya awali, pamoja na nyimbo mbili mpya zilizoandikwa na Stephen Schwartz mwenyewe — mtunzi wa original musical.
"For Good" pekee tayari ime-pita zaidi ya million 45 plays kwenye Spotify — proof kwamba fanbase ya Wicked bado iko strong, na duet hii ina-hit emotionally kwa jinsi ambavyo movie yenyewe ina-close hadithi.
Weka hii kwenye playlist yako leo — hasa kama ulilia kwenye sinema wakati wa scene hii.
Chanzo: BongoScreen