TV spots mpya za Clayface zinaonyesha kuwa DCU wanaingia horror territory kwa mara ya kwanza, wakificha full transformation ya villain kujenga hype zaidi.
DCU wana-cook kitu tofauti kabisa na tunachozoea, na hii mara wanaingia kwenye horror territory kupitia filamu ya Clayface. TV spots mpya zimeshaanza kutoka na zinaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa hii itakuwa filamu ya kwanza ya horror ndani ya DCU mpya inayoongozwa na James Gunn na Peter Safran.
Kinachovutia zaidi ni jinsi trailer inavyocheza na mawazo ya watazamaji. Badala ya kuonyesha full transformation ya villain mara moja, wamechagua kuficha, wakitupa vipande tu vya body-horror vinavyofanya Clayface aonekane creepy na wa kutisha kuliko tulivyozoea kumuona kwenye comics au animated series. Ni move ya kimkakati — kujenga hype huku wakiacha reveal kubwa kwa premiere.
Gotham tunayoifahamu kwenye Batman movies mara nyingi inaonyeshwa kama jiji la crime na noir aesthetic, lakini hapa DCU wanaonyesha side nyingine kabisa — moja yenye giza la kisaikolojia na body-horror elements ambazo hazijawahi kuguswa sana kwenye big screen za DC. Hii inaonyesha jinsi studio inavyotaka kupanua genre range ya universe yao, wasibaki tu kwenye superhero action za kawaida.
Wazo la kuleta horror ndani ya DCU si jambo dogo. Kwa muda mrefu, mashabiki wamekuwa wakisubiri DC iwe na ujasiri wa kuchezea genres tofauti kama ambavyo Marvel walijaribu na miradi kama Werewolf by Night. Clayface inaonekana ndiyo itakuwa jibu la DC kwa hilo swali, ikiwa first real test ya kama universe hii mpya inaweza kubeba stories za aina tofauti bila kupoteza identity yake ya msingi.
Kwa sasa, taarifa kamili za full look ya monster bado hazijatoka, jambo linaloonyesha marketing team wana strategy ya kuweka mystery hai mpaka siku ya release. Hii ni classic horror marketing playbook — usimwoneshe monster mzima mapema, waache watazamaji wajenge fear kwenye vichwa vyao wenyewe.
Kwa mashabiki wa DC wanaotamani kuona universe ikichukua risks mpya, hii trailer ni ishara njema. Tutaendelea kufuatilia kadri taarifa zaidi zinavyotoka kuhusu Clayface na jinsi itakavyobadilisha mtazamo wa Gotham ndani ya DCU.
Chanzo: GamesRadar